Usa River Rehabilitation and Training Centre

We believe in your ability!

  • Schrift vergrößern
  • Standard-Schriftgröße
  • Schriftgröße verkleinern
Usa River Rehabilitation and Training Centre

Karibu kwenye mtandao wetu

Chuo chetu ni mahali ambapo watu wenye ulemavu na wasiokuwa na ulemavu wanaishi na kufanya kazi pamoja na kwa ushirikiano “Tunaamini unaweza” ni mwongozo wautendaji na mafikira yetu. Tunaamini unaweza - Sentensi hii ina madhumuni matatu kwetu:

  1. Tunaamini unaweza - Kuishi maisha ya kujitegemea

    Kuishi kama mlemavu Tanzania, nchi maskini sana hapa duniani ni vigumu sana
    Hamna msaada kutoka kwenye serekali kwenye msimu wa joto walemavu huishi kwenye vumbi na kwenye msimu wa mvua huishi kwenye tope. Uwezo wa kupata elimu ni mgumu na hata wakati mwingine wanakosa elimu kabisa. Hii ni kwa sababu ya kipato kidogo cha familia yenye watoto sita au nane. Takwimu zinaonyesha kwamba mapato ya Mtanzania ni chini ya Shs.1000  kwa siku. Mpaka sasa watoto walemavu wanaonekana kama alama ya aibu na wanafichwa vijijini. Na tunaamini kwamba walemavu wengi kama wakipewa nafasi,wanauwezo wa kubadilisha maisha yao kuwa mazuri. Ndio maana tunataka kila mwanafunzi aelewe:

    Anaweza kupata maisha mazuri. Tunaamini unaweza!

  2. Tunaamini unaweza –Tajiri kutumia utajiri wako kwa ukarimu

    Familia nyingi hawana uwezo wa kulipa ada ya shule. Hata hivyo bado tunawapokea vijana wao kwenye chuo chetu. Lakini tunafanya hivyo kwa sababu kuna watu wanaojitolea kutupa msaada kwenye kazi hii. Hatuombi, lakini tunaamini kwamba ni vizuri watu matajiri wakianza kusaidia wengine kutokana na utajiri wao.  Tunahitaji kila mchango kidogo na tutashukuru sana tukiupata.  Pia, kwa wale matajiri tunasema:

    Tunaamini unaweza!

  3. Tunaamini unaweza -Na tunamtumaini Mungu kwa ajili yako

    Ni kweli kuna walemavu wengine huwa na maumivu Makali, na hutengwa na jamii, wana umaskini, hawawezi kuvumilia matatizo yao. Na sisi kama wasaidizi tunasema... kama mtu akikosa ujasiri, tunayatumainia matendo makuu ya Mungu. Kwamba anaponya. Kwamba anatupa nguvu. Kwamba anatufariji.

    Tunataka kumwambia Mungu pia.
    Tunaamini anaweza!

Claus Heim & Sophia Moshi